IQNA

Nakala ya Qur'ani yenye umri wa miaka 500 kuonyeshwa kwenye intaneti

10:11 - January 23, 2011
Habari ID: 2068960
Msemaji wa Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza amesema kuwa chuo hicho kitaonyesha nakala nadra ya Qur'ani iliyoandikwa kwa hati za mkono yapata miaka 500 iliyopita.
Msemaji wa Chuo Kikuu cha Manchester amesema nakala hiyo ya Qur'ani iliandikwa miaka 500 iliyopita na ina thamani kubwa mno. Amesisitiza kuwa karatasi za nakala hiyo ya Qur'ani zimezeeka sana na ni dhaifu kwa kadiri kwamba wataalamu wameshindwa kuionyesha hadharani kwa watu.
Amesema kuwa nakala hiyo ya Qur'ani inahifadhiwa katika maktaba ya John Rylands ya Chuo Kikuu cha Manchester huko kaskazini mwa Uingereza na ina kurasa 470 zenye ukubwa wa sentimita 60 kwa 88 sawa na ukubwa wa televisheni ya pasma.
Ameongesa kuwa wataalamu wa maktaba hiyo wana nia ya kutumia teknolojia ya digitali kupiga picha kurasa za nakala hiyo adimu ya Qur'ani na kuichapisha kwenye mtandao wa intaneti kwa ajili ya kutumiwa na wanachuo na wahadhiri wa vyuo vikuu.
Wataalamu wanasema nakala hiyo ya Qur'ani iliandikwa katika nusu ya pili ya karne ya 14 hadi mwanzoni mwa karne ya 15.
Wanahistoria wanasema kuwa nakala hiyo ya thamani ya Qur'ani ilibakia katika maktaba ya Qansura al Gharawi, mfalme wa mwisho wa utawala wa Mamalik nchini Misri. 734491
captcha