Aidha amempongeza Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran kwa sisitizo lake la kuundwa umoja huo.
Ameongeza kuwa Iran ndio nchi bora zaidi inayoweza kuanzisha muungano huo.
Ustadh Al Musalmani ambaye alikuwa katika jopo la majaji wa Mashindano ya Tatu ya Qur'ani ya Kimataifa ya Wanachuo Waislamu ametaja kiwango cha mashindano hayo kuwa cha juu na kuongeza kuwa washiriki walikuwa wamejitayarisha vizuri.
Msomi huyo wa Lebanon amesema kuwepo maustadhi wa Qur'ani kama vile Abul Ainain Shu'aisha na Ahmad Ahmad Nuaina kutoka Misri na vilevile wataalamu wa Qur'ani kutoka Iran ni jambo lililohakikisha kuwa mashindano hayo yanabakia katika kiwango cha juu.
Ustadh Al Musalmani ambaye ni hafidh wa Qur'ani nzima amepongeza hatua ya mashindano ya Qur'ani kufanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad. Aidha amewashukuru waandalizi kwa kuandaa maonyesho ya Qur'ani pembizoni mwa mashindano hayo.
Mashindano ya Tatu ya Qur'ani ya Kimataifa ya Wanachuo Waislamu yalifanyika Januari 9-11 katika mji mtakatifu wa Mash'had kaskazini-mashariki mwa Iran na kuhudhuriwa na wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi 40 duniani.
734743