Gazeti la Saudi Gazette linalochapishwa nchini Saudi Arabia limeandika kuwa jumla ya vitabu milioni 1.3 vinahifadhiwa katika maktaba ya Mfalme Abdul Aziz na zaidi na vitabu elfu 32 vilichapishwa katika kipindi cha kuanza zama za chapa barani Ulaya.
Orodha ya vitabu vya maktaba hiyo inajumuisha vitabu nadra 78 kuhusu maisha ya Mtume Muhammad (saw) na tarjumi 113 za Qur'ani kwa lugha tofauti za Ulaya zlizochapishwa na na taasisi mbalimbali barani humo.
Maktaba hiyo pia ina vitabu nadra vya kisayansi na kihistoria vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu katika karne ya 16 Miladia. Kitabu muhimu zaidi kati ya vitabu hivyo ni kile cha mwanafalsafa na tabibu mashuhuri wa Kiislamu wa Iran Abu Ali Sina.
Maktaba ya Mfalme Abdul Aziz ya Riyadh pia ina nakala zilizoandikwa kwa hati za mkono, nyaraka nadra na zaidi ya vitabu elfu tatu vilivyoandikwa kwa lugha za kigeni kuhusu matukio ya kihistoria na kisiasa ya nchi za Ghuba ya Uajemi. 739532