IQNA

Qari Mtanzania ataka washiriki wa mashindano ya Qurani waongezeke

13:49 - February 03, 2011
Habari ID: 2074646
Qari kutoka Tanzania aliyeshiriki katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani ya Wanachuo waislamu amesema kiwango cha mashindano kilikuwa cha kuridhisha na ametoa wito kwa waandalizi kuongeza idadi ya washiriki.
Hussein Hassan Abdullah aliyewakilisha Tanzania katika mashindano hayo yaliyofanyika Januari 9-11 mjini Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.
Hassan Abdullah ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa mashindano hayo ya Qurani.
Akiashiria harakati za Qurani nchini Tanzania, amesema harakati hizo zinatokana na utamaduni wa Watanania. Ameongeza kuwa Waislamu wa Tanzania wamepiga hatua katika uga wa Qurani katika miaka ya hivi karibuni.
Amesema mashindano ya kimataifa ya Qurani hufanyika nchini Tanzania kila mwaka. Hassan Abdullah mwenye umri wa miaka 18 amesema alianza kusoma Qurani Tukufu akiwa na umri wa miaka minne. Amesema hii ndio safari yake ya tatu nchini Iran na amewataka Wairani kuwa watu wakarimu.
739472
captcha