IQNA

Mashindano ya kitaifa ya hifdhi na tajwidi ya Qur'ani Tukufu yamalizika Mali

13:28 - February 05, 2011
Habari ID: 2075228
Duru ya kwanza ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi na tajwidi ya Qur'ani Tukufu ambayo yalianza tarehe 25 Januari huko Bamako mji mkuu wa Mali yalimalizika siku ya Alkhamisi tarehe Februari 3.
Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na Shirika la Huduma za Kibinadamu la As-Sheikh Thani bin Abdallah la Qatar yalifanyika kwa ushirikiano wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mali na Taasisi ya Masuala ya Kheri ya Kiislamu ya nchi hiyo kwa jina la al-Farouq pamoja na msaada wa Waziri Mkuu wa Mali.
Duru ya kwanza ya mashindano hayo imewashirikisha washindani 57 katika makundi mawili ya wanawake na wanaume kutoka mikoa yote minane ya nchi hiyo ya Kiafrika.
Sherehe ya kuhitimisha mashindano hayo imefanyika katika ukumbi mkuu wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Mali katika mji wa Bamako ambapo washindi wametunukiwa zawadi nono na za kuvutia. 741389
captcha