Tovuti ya Tribune imeripoti kuwa Haroun Wakili ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya jimbo la Jigawa amesema inatazamiwa kuwa washiriki 550 kutoka majimbo 30 ya Nigeria na wageni na wasimamizi makhsusi 1000 watashiriki katika mashindano hayo.
Haroun Wakili amesema jimbo la Jigawa limechukua uamuzi wa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa shabaha ya kuimarisha sera zake za kustawisha zaidi elimu na taaluma za Kiislamu na kudhihirisha uwezo wake wa kuwa mwenyeji wa matukio kama hayo ya kitaifa na kimataifa.
Ameongeza kuwa moja ya malengo ya mashindano hayo ya Qur'ani ni kuwahamasisha vijana wa Kiislamu kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu na vilevile kuimarisha umoja na mshikamano kati ya Waislamu.
Wakili amesema anatarajia kwamba mashindano hayo pia yataboresha usomaji wa Qur'ani wa wanafunzi wa shule na vyuo vikuu. 741439