IQNA

Utekelezwaji sahihi wa mafundisho ya Qur'ani, suluhisho la matatizo ya jamii

13:53 - March 08, 2011
Habari ID: 2092224
Utekelezwaji sahihi wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu pamoja na ya Mtume (saw) ni njia bora zaidi ya kutatua matatizo mengi yanayoikabili jamii ya Kiislamu, yakiwemo ya umasikini, ughali wa maisha, hongo na ufisadi.
Kwa mujibu wa tovuti ya Two Circles, maneno hayo yametamkwa na Javid Mukarram, mwanafikra wa Kiislamu wa India katika kikao cha Sira ya Mtume kilichofanyika huko Jaipur makao makuu ya Jimbo la Rajesthan nchini India.
Huku akibainisha kwa kina mafundisho ya Qur'ani kuhusiana na suala la uchumi, Mukarram amesema kutokana na kutegemea riba, mifumo ya kiuchumi isiyokuwa ya Kiislamu hupelekea watu masikini kuwa masikini zaidi na matajiri kuwa matajiri zaidi na hivyo kupanua pengo la matabaka hayo mawili katika jamii. Ameongeza kwamba India inahitaji kuwa na mfumo wa kifedha usio wa riba ili kumuwezesha kila mtu kunufaika kwa mujibu wa juhudi zake.
Wasomi wengine wa Kiislamu wa India walioshiriki katika kikao hicho pia walitoa mitazamo na maoni yao kuhusiana na ubora wa mafundisho ya Kiislamu katika kutatua matatizo ya jamii ya Kiislamu na isiyo ya Kiislamu.
Kikao hicho kimeandaliwa na Jamii ya Kiislau ya mji wa Jaipur. 759165
captcha