Wajumbe wa Baraza Kuu la Qur'ani wamepokelewa na Abdul Rauf Changi Zehi ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Othmaniya na mkurugenzi wa Chuo cha Kidini cha Faruqiah.
Kikao hicho kilichoanza na kisomo cha Qur'ani Tukufu kilikuwa fursa nzuri kwa pande mbili kujadili masuala ya Qur'ani katika mazingira ya kirafiki.
Safari hiyo ni katika fremu ya safari za wajumbe wa Baraza Kuu la Qur'ani la Iran katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kutafuta watu wenye vipawa vya Qur'ani, kukagua vituo cha Qur'ani na kuwaenzi wale wanaohudumia kitabu hicho kitakatifu hapa nchini.
761807