Rahman Malik, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan ameiandikia barua polisi ya kimataifa ya Interpol akiitaka ifuatile kwa karibu wahalifu waliohusika na uchomaji Qur'ani Tukufu huko katika jimbi la Florida nchini Marekani.
Kwa mujibu wa tovuti ya The News, Waziri Malik amesema kuwa kitendo cha kasisi muovu Terry Jones cha kuchoma kwa mara ya pili Qur'ani Tukufu ni cha kigaidi ambacho kinapaswa kufutiliwa kisheria ili kuzuia kukaririwa tena. Amesema kwa kitendo chake hicho kiuvu, si tu kwamba Terry Jones amewaudhi Waislamu wa Pakistan tu bali Waislamu wote katika pembe zote za dunia. Tunakumbusha hapa kuwa siku ya tarehe 20 Machi Kasisi Terry Jones wa kanisa la Dove World Outreach Center katika mji wa Gaineville jimboni Florida alisimamia kitendo cha kuaibisha na cha dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu, cha kuchomwa kitabu kitakatifu cha Qur'ani mbele ya watu walio na chuki dhidi ya Uislamu ambao pia walipiga picha kitendo hicho cha kuchukiza. Kitendo hicho kimewakasirisha sana Waislamu katika pembe zote za dunia. 766714