IQNA

Ombi la kuanzishwa chuo cha muujiza wa kielimu wa Qur'ani nchini Misri

11:35 - March 31, 2011
Habari ID: 2099293
Washiriki wa sherehe za kuwaenzi washindi wa mashindano ya kimataifa ya muujiza wa kielimu wa Qur'ani na sunna za Mtume Mtukufu (saw) ambazo zilifanyika hapo siku ya Jumanne huko katika mji mkuu wa Misri Cairo, wametaka kuasisiwa kwa chuo cha muujiza wa kielimu wa Qur'ani nchini humo.
Sherehe hizo zilizohudhuriwa na Ahmad Tayyib, Sheikh wa al-Azhar, ziliwaenzi washindi wa mashindano ya kimataifa ya muujiza wa kielimu wa Qur'ani yaliyofanyika mwaka jana wa 2010. Maustadh mashuhuri wa mafunzo na usomaji Qur'ani wa Misri walishiriki katika sherehe hizo na kutoa hotuba zao kuhusiana na muujiza wa kielimu wa Qur'ani Tukufu katika taaluma mbalimbali. Washiriki wa sherehe hizo pia wametaka kuanzishwa somo maalumu la muujiza wa kielimu wa Qur'ani katika mifumo ya masomo ya nchi hiyo. Sherehe hizo ziliandaliwa na Chuo Kikuu cha al-Azhar kwa ushirikiano wa Benki ya Kiislamu. 767229
captcha