Kongamano hilo limeandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu na vilevile Kamati ya Kitaifa ya Elimu, Utamaduni na Sayansi ya Sudan. Lengo la kufanyika kongamano hilo limetajwa kuwa ni kunyanyua kiwango cha masomo katika taasisi za Qur'ani, kutathmini shughuli za taasisi hizo na kutumiwa suhula za kisasa ikiwemo intaneti na kanali za satalaiti katika kuboresha masomo ya taasisi hizo. 767833