Kikao hicho kimeandaliwa na Jumuiya ya Qur'ani ya Oxford. Kwa mujibu wa tovuti ya Quran-institute, tafsiri na wafasiri, historia fupi ya uchapishaji Qur'ani, sanaa na kaligrafia katika nuskha za Qur'ani, Qur'ani katika mtandao wa intaneti, matukio na shughuli za Qur'ani duniani ni baadhi ya maudhui zitakazochunguzwa na kujadiliwa katika kikao hicho. Walio na hamu ya kushiriki katika kikao hicho wana muda wa hadi kufikia tarehe 18 Mei kuwasilisha utangulizi wa makala zao kupitia anwani ifuatayo ya intaneti: Submit@quran-institute. Org.uk. Iwapo utangulizi huo utakubaliwa basi wataombwa kuwasilisha makala kamili kwa taasisi hiyo kufikia tarehe 18 Juni. Utangulizi wa makala hizo unapasa kuwa kati ya maneno 400 hadi 500 na makala kamili kati ya maneno 3000 hadi 3500. Kikao cha kwanza cha utafiti huo wa Qur'ani kilifanyika katika chuo hicho Agosti 16 na 17 mwaka 2009. 769071