IQNA

Usambazaji Qur'ani wazuiwa Palestina kutokana na makosa ya chapa

12:01 - April 12, 2011
Habari ID: 2104575
Sheikh Muhammad Hussein, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mamufti ambaye pia ni Mufti Mkuu wa Palestina na Quds Tukufu amezuia kusambazwa kwa nuskha za Qur'ani Tukufu huko Palestina kutokana na makosa ya chapa yaliyomo humo.
Akizungumzia suala hilo, Sheikh Muhammad Hussein amezitaka taasisi, maktaba na mashirika yote ya uchapishaji na usambazaji pamoja na watu walio na Qur'ani hiyo iliyo na makosa ya chapa kuikabidhi kwa vituo vya Dar al-Iftaa vilivyo karibu nao. Mufti mkuu huyo amewataka watu wote wanaohusika na uchapishaji pamoja na usambazaji wa Qur'ani Tukufu kuwa waangalifu zaidi wanaposambaza kitabu hicho kitakatifu. 772922
captcha