Zahra Malali bint Mohammad Nader ameenziwa katika sherehe zilizohudhuriwa na wabunge. Alitunukiwa zawadi ya takribani Euro 500 katika hafla iliyoanza kwa kisomo chake cha Qurani.
Wabunge pia wamependekza hafidh huyo wa Qurani nzima atunukiwe nishani ya Seyyed Jamaluddin Afghani ambayo ni kati ya nishani ya juu zaidi nchini humo.
Zahra Malali alianza kuhifadhi Qurani akiwa na umri wa miezi 16 chini ya Ustadh Fadhl Bari, hafidh wa Qurani nzima kutoka Madrassah ya mjini Naveh mkoani Helmand.
774481