IQNA

Kikao cha 'Juhudi za Umma wa Kiislamu za Kuhudumia Qur'ani' chamalizika Morocco

17:02 - April 17, 2011
Habari ID: 2107229
Kikoa cha kimataifa cha 'Juhudi za Umma wa Kiislamu kwa ajili ya Kuhudumia Qur'ani Tukufu na Taaluma ya Qur'ani' kilianza jana Jumamosi tarehe 16 Aprili katika mji wa Fes nchini Morocco.
Kwa mujibu wa maroccjounal.net lengo la kufanyika kikao hicho cha siku mbili ambacho kinamalizika leo Jumpili ni kuchunguza utafiti wa Kiislamu na uzoefu uliopatikana kwa ajili ya kuwasilishwa kwa kizazi kijacho na kuhuisha pamoja na kueneza vyema ujumbe wa Mwenyezi Mungu katika uwanja huo. Kutathminiwa shughuli za ulimwengu wa Kiislamu katika uwanja wa kuhudumia Uislamu na Qur'ani Tukufu ni malengo mengine ya kuandaliwa kikao hicho. Juhudi za umma wa Kiislamu katika kueneza ujumbe wa Kiislamu katika karne zilizopita pia ni jambo jingine ambalo limechunguzwa katika kikao hicho kilichoandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Muujiza wa Kielimu wa Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume (saw) kwa ushirikiano na Jumuiya ya Maulama, Chuo cha Sayyid Muhammad bin Abdallah, Taasisi ya Utafiti wa Kielimu ya Fes pamoja na Taasisi ya Utafiti ya Morocco. 775700
captcha