Nuskha 553,000 zisizo na kibali cha chapa kutoka kwa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya al-Azhar zimekusanywa na Idara Kuu ya Uchunguzi wa Chapa na Uteteaji wa Haki Miliki ya Kimaanawi ya Wamiliki huko mjini Cairo.
Inasemekana kuwa mkuu wa kituo kilichochapisha Qur'ani hizo ametiwa nguvuni kwa ajili ya kusailiwa kuhusiana na hatua yake ya kuchapisha Qur'ani hizo bila kupata kibali kutoka kwa idara husika. Idara iliyotajwa pia imekusanya kopi 1000 za vitabu vingine vya masomo vilivyochapishwa kinyume cha sheria bila kupata idhini ya waandishi, na kumtaka mwendesha mashtaka mkuu wa Misri kuwachukulia hatua wahalifu. Mkuu wa idara hiyo amesema kuwa idara yake imaimarisha juhudi za kusaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahalifu wote wanaokiuka sheria za haki miliki kwa madhara ya waandishi wa vitabu. 776152