IQNA

Mwanakaligrafia mchanga zaidi wa Qur'ani katika kikao cha Madina

17:06 - April 25, 2011
Habari ID: 2111810
Kikao cha Kimataifa cha Wanakaligrafia wa Qur'ani Duniani kitafanyika Aprili 26 katika mji wa Madina ambapo kijana mwenye umri wa miaka 13 kutoka Algeria, Mohammad Humam Al Shebl, ndiye mshiriki mwenye umri mdogo zaidi.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan, mwanakaligrafia mwenye umri wa miaka 92 kutoka Misri, Mohammad Ebrahim Salamah, ndiye mshiriki mwenye umri wa juu zaidi katika kikao hicho.
Kikao hicho kimeandaliwa na Kituo cha Uchapishaji cha Malik Fahd na kitaendelea hadi Mei pili.
Washiriki watajifunza kuhusu historia ya kaligrafia ya Qur'ani tokea zama za Mtume Muhammad SAW hadi sasa.
Kikao hicho cha kimataifa kinalenga kuwaenzi wanakaligrafia wa Qur'ani na kuwawezesha kubadilishana mawazo kuhusu fani yao.
779844
captcha