IQNA

Madai ya kuwepo makosa katika tarjumi ya Qur'ani yakanushwa Indonesia

17:58 - April 26, 2011
Habari ID: 2112642
Wizara ya Masuala ya Dini ya Indonesia imekanusha madai yaliyotolewa na Baraza la Wanajihadi wa Kiindonesia (MMI) kwamba kuna makosa katika zaidi ya nusu ya tarjumi za Qur'ani nchini humo.
Kituo cha upashaji habari cha Tempointeractive kimemnukuu Nasruddin Umar ambaye ni Mkurugenzi wa Jumuiya ya Mwongozo wa Kiislamu ya Indonesia akisema kuwa madai ya kuwepo makosa katika tajumi ya Qur'ani ambayo inasemekana kuwa yanapanua zaidi ugaidi hayana msingi wowote na yanaeneza mbegu za unafiki kati ya Waislamu. Amesema tarjumi ya Qur'ani Tukufu inasimamiwa na timu ya watarjumi wa Qur'ani ya Wizara ya Masuala ya Dini ya Indonesia ambayo inajumuisha wawakilishi wa taasisi muhimu. Ameongeza kuwa idadi ya aya ambazo inadaiwa kuwa zimetarjumiwa kimakosa ni zaidi ya asilimia 50 ya Qur'ani nzima. Amehoji kwamba Majlisi ya Wanajihadi Waindonesia imetegemea kitu gani katika kutoa madai kama hayo?
Nasruddin Umar amesema jumuiya yake iko tayari kwa ajili ya kuchunguza madai hayo na kuongeza kuwa tarjumi mpya ya Qur'ani Tukufu imechapishwa na Idara ya Utafiti na Ustawi ya Wizara ya Masuala ya Dini ya Indonesia. 781340
captcha