Katika tafsiri yake iliyoandikwa kwa muhtasari lakini yenye faida tele, Allamah Muhammad Jawad Mughnia amebainisha masuala ya balagha na fasihi ya Qur'ani na kufichua muujiza wa aya za kitabu hicho, mbinu ambayo inashabihiana na ile iliyotumiwa na Allamah Zamakhshari katika tafsiri ya al Kashaf.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Kiislamu cha Karbala nchini Iraq Abdul Amir Kadhim Zahid akijibu swali kwamba ni kwa nini tafsiri ya al Mubin ikatambuliwa kuwa moja na tasiri bora za Imammiya katika karne ya hivi karibuni?
Amesema sababu ni mbinu ya Allamah Mughnia ya kutilia maanani balagha na fashi, sentensi fupi, kutumia misingi ya kufichua siri za ibara na aya za Qr'ani na kuchunguza muujiza wa kitabu hicho.
Amesema mbinu hiyo inafanana na ile iliyotumiwa na Allamah Zamakhshari katika tafsiri ya al Kashaf.
Katika sehemu nyingine ya mazungumzo yake Dakta Zahid amesema tafsiri zote mbili za al Mubin ya Allamah Mughnia na ile ya al Kashaf ya Allamah Zamakhshari zimefaidika na maudhui mbalimbali na zote zimetilia maanani masuala ya lugha, fasihi na balagha. 784440