IQNA

Tovuti ya Tazim-ul-Qur'an yazinduliwa Madina

14:18 - May 10, 2011
Habari ID: 2119561
Tovuti ya Tazim-ul-Qur'an imezinduliwa katika mji mtakatifu wa Madina pembizoni mwa sherehe za kuwaenzi washindi wa mashindano ya Qur'ani yaliyofanyika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Imad Zahir Hafez mkuu wa mpango wa Tazim-ul-Qur'an amesema lengo lake ni kubainisha nafasi ya juu ya Qur'ani Tukufu, kuelezea miujiza ya kitabu hicho na kuwafahamisha Waislamu majukumu yao kuhusu Qur'ani.
"Kuwaelimusha watoto kuhusu nafasi ya Qur'ani na kuwahimiza kuimarisha uhusiano na kitabu hicho kitukufu, kuwaonya Waislamu kuhusu hatari za kuiacha Qur'ani na kukilinda kitabu hiki kitukufu kutokana na hujhuma za maadui ni kati ya malengo mengine ya mpango huu", amesema.
Ameelezea matumaini yake kuwa mpango wa Tazim-ul-Quran utakuwa mfano wa kuigwa katika ustawishaji wa mafundisho na thamani za Qur'ani Tukufu.
788426
captcha