Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na Dr Madeeha bint Ahmed al Shibaniyah Waziri wa Elimu na Malezi wa Oman ilishuhudia wanafunzi watano bora walioshinda mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu wakitunukiwa zawadi na kuenziwa na wasimamizi pamoja na waandaaji wa mashindano hayo.
Mafunzo ya Qur'ani katika shule zote za serikali na zisizo za serikali, juhudi za kueneza utamaduni wa Kiislamu katika shule hizo, kuandaliwa mazingira bora ya hifdhi na usomaji Qur'ani shuleni, kushajiishwa wanafunzi wasome na kuhifadhi Qur'ani, kuandaliwa mashindano ya Qur'ani na uimarishwa wa lugha ya Kiarabu kwa lengo la kushiriki katika mashindano hayo ni baadhi ya mambo yaliyosisitizwa katika sherehe hiyo.
Mashindano hayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka nchini humo. 788848