Nakala hizo za Qur'ani zimetolewa na watetezi wa mazingira wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Risalat ya Misri.
Msemaji wa Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Risalat Marwa Abdul Maqsud amesema kuwa jumuiya hiyo imetuma Qur'ani hizo baada ya kugundua kwamba Waislamu wa nchi hizo za Afrika Kusini, Ivory Coast na Niger wanakabiliwa na uhaba wa nakala za Qur'ani Tukufu.
Jumuiya ya masuala ya kheri ya Risalat ya Misri ni miongoni mwa taasisi kubwa zaidi zenye matawi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na hujishughulisha zaidi na kutoa misaada kwa wahitaji, mayatima na watu wenye maradhi makhsusi. 791829