IQNA

Nakala yenye umri wa miaka 900 ya Qur'ani yagunduliwa Pakistan

14:29 - May 18, 2011
Habari ID: 2124089
Nakala ya Qur'ani Tukufu yenye umri wa miaka 900 ambayo iliandikwa katika karne ya 12Miladia imegunduliwa katika mji wa Jhelum nchini Pakistan.
Kituo cha habari cha Tribune kimeripoti kuwa nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu yenye thamani kubwa iligunduliwa na mtaalamu wa mambo ya kale wa Pakistan katika safari yake kwenye mji wa Jhelum katika mkoa wa Punjab.
Nakala hiyo ya Qur'ani ya kale iliandikwa na Sirajuddin Abu Tahir Muhammad bin Abdul Rashid katika karne ya 12 Miladia.
Nakala hiyo iliyoandikwa kwa hati za mkono ina uzito wa karibu kilo tano na kurasa 1200 na wino wa baadhi ya kurasa zake umefifia kutokana na umri wake mkubwa.
Wataalamu wanakadiria kwamba nakala hiyo ya thamani kubwa ya Qur'ani iliandikwa na watu watatu katika kipindi cha mwaka mmoja. 793520
captcha