Gazeti la The News limeripoti kuwa maandamano hayo yaliyoongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mawakili wa Swabi Ahmad Alikhan yamelaani watu waliohusika na kitendo hicho kiovu.
Ahmad Alikhan ametoa hotuba katika mkusanyiko huo akitaka kuchukuliwa hatua za kisheria waliousika na uhalifu huo.
Tarehe 17 Mei kundi moja la watu wasiojulikana lilichoma moto nakala 80 za kitabu kitakatifu cha Qur'ani, suala ambalo limezusha wimbi kubwa la hasira kati ya wakazi wa mji wa Swabi nchini Pakistan.
Kundi hilo lilishambulia shule moja ya Kiislamu katika eneo hilo na kuteketeza kwa moto nakala za Qur'ani Tukufu.
Polisi ya Pakistan imeanza uchunguzi wa kuwasaka watu waliotekeleza uhalifu huo. 795662