Masomo hayo ya muda mfupi yanadhaminiwa na Kitengo cha Vituo vya Hifdhi ya Qur'ani cha Maktum kinachofungamana na Idara ya Taasisi za Kiislamu inayofungamana na Idara ya Masuala ya Kiislamu na Kheri ya Dubai.
Akizungumzia suala hilo Muhammad al-Abri, mratibu wa kituo hicho amesema kuwa masomo hayo ambayo yamegawanywa katika sehemu 94 yatafanyika katika Msikiti Mkuu wa az-Zarqaa na misikiti mingine ya Imarati. Amesema kuenezwa utamaduni wa Kiislamu na Qur'ani katika matabaka mbalimbali ya jamii ya Imarati na kuwafahamisha wanafunzi maarifa ya Kiislamu na Qur'ani Tukufu ni moja ya malengo ya kitengo hicho. 798582