IQNA

Vituo vya kuwafunza wataalamu bingwa wa Qu’rani kuanzishwa Iran

10:10 - May 30, 2011
Habari ID: 2130473
Vituo 31 vya kutoa mafunzo kwa wataalamu bingwa wa Qur’ani Tukufu vitaanzishwa katika mikoa yote 31 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Utafiti katika Taasisi ya Darul Qur’an nchini Iran Bw. Dawud Takfallah ambaye amesema vituo 6 vya kwanza vitazinduliwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Amesema vituo hivyo vitasimamiwa na wanazuoni mashuhuri wa Qur'ani katika kila mkoa.
Bw. Takfallah amesema Taasisi ya Darul Qur'an itabuni kitengo cha kutafuta wenye vipawa vya Qur’ani na kuwapa mafunzo baada ya hapo.
799717
captcha