Haya ni kwa mujibu wa Hujjatul Islam Ahmad Ahmadi mwanachama wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni nchini Iran ambaye pia ni mkuu wa Shirika la Utafiti na Uandishi wa Vitabu vya Masomo ya Kijamii ya Vyuo Vikuu. Aliyasema hayo katika kikao cha kutathmini tarjumi za Kiingereza za Qur’ani Tukufu kilichofanyika katika makao makuu ya IQNA mjini Tehran Mei 21.
‘Mtarjumi wa Qur’ani aliyehitimu anapaswa kufahamu vyema matukio ya kihistoria ya zama za Mtume SAW na kufasiri sababu na wakati wa kushuka aya mbalimbali ili kwa njia hiyo aweze kufikisha kwa njia halisi ujumbe wa Wahyi kwa wasomaji’, ameongeza.
Amesema, kuwa na ujuzu wa fiqhi na mbinu mbalimbali za usomaji pamoja na kufahamu filosofia na sayansi za msingi ni kati ya masharti mengine ya mwenye kutarjumi Qur’ani.
Amenukulu mtarjumi wa moja kati ya tarjumi bora za Qur’ani kwa lugha ya Kiingereza John Arthur Arberry aliyesema, ‘Qur’ani inapotarjumiwa kwa lugha nyingine hupoteza umaridadi wake wakati wa kufikisha ujumbe wake kwa lugha kusudiwa’. Hujjatul Islam Ahmadi amesema kutarjumi Qur’ani kwa lugha nyinginezo ni jambo la dharura na kwa hivyo kuna haja ya kujitahidi kuhakikisha kuwa ujumbe wake unafikishwa kwa lugha inayofahamika.
799331