Zamir Akram ambaye alikuwa akizungumza kwa niaba ya nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) amemkosoa vikali Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa akisema katika taarifa aliyotoa hivi karibuni hakuashiria hata kidogo vitendo vya kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini Marekani.
Ameongeza kuwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa hakusema lolote kuhusu maafa ya kuchomwa moto Qur'ani katika jimbo la Florida huko Marekani, suala ambalo limezusha wimbi kubwa la hasira na hali ya mivutano kati ya wafuasi wa dini mbalimbali.
Akram amesema, kuongezeka vitendo vya ubaguzi wa kidin si jambo linaloweza kunyamaziwa kimya na kuna udharura kwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa kulipa kipaumbele suala hilo katika ajenda ya kazi zake. 801545