Hatua hiyo imechukuliwa baada ya malalamiko makali ya Waislamu wa Ubelgiji.
Kituo cha habari cha 7sur7 kimeripoti kuwa maduka makubwa ya Carrefour yameamua kusimamisha uuzaji wa karatasi hizo za shashi zenye nakshi ya jina tukufu la Mtume Muhammad (saw) na jila la Mwenyezi Mungu la Allah baada ya Waislamu wa Ubelgiji kuwasilisha malalamiko makali dhidi ya kitendo hicho.
Waislamu wa Ubelgiji waliripoti suala hilo kwa maimami wa misikiti na baadaye jumuiya za Kiislamu zikawasilisha mashtaka dhidi ya kampuni iliyotengeneza makaratasi hayo ya kujifutia uchafu. 801471