IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani Tukufu mjini Asyut Misri waenziwa

18:11 - June 01, 2011
Habari ID: 2132504
Washindi wa masindano ya kila mwaka ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu mjini Asyut Misri walienziwa hapo jana Jumanne tarehe 31 Mei.
Mashindano hayo ambayo yamewashirikisha vijana wa kike na kiume wapatao 1600 yameandaliwa na Idara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Asyut inayofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri.
Muhammad Izzu Deen, mwakilishi wa wizara iliyotajwa katika mashindano hayo amesema kuwa yamefanyika katika sehemu nne za hifdhi ya Qur'ani nzima, hifdhi ya thuluthi tatu, juzuu 15 na hifdhi ya robo moja ya Qur'ani Tukufu. Amesema kati ya washiriki, vijana 55 walichaguliwa kuwa washindi wa mashindano hayo na kupewa fursa ya kushiriki katika hatua ya baadaye na mashindano hayo ambayo ni ya kitaifa na ambayo yamepangwa kufanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani huko Cairo mji mkuu wa Misri.
Amesema washindi wa mashindano hayo ya hifdhi ya Qur'ani watatangazwa katika usiku wa Leilatul Qadr na kutunukiwa zawadi na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri. Washiriki wa mashindano ya Asyut ni watoto na vijana wenye umri wa kati ya miaka 6 hadi 21. 802300
captcha