Mpango huo wa kugawa nakala za kitabu kitukufu cha Qur’ani unaotekelezwa na Jamat Islamiya, unafanyika kwa lengo la kutaka kuwaelimisha Wahindu kuhusu kitabu kitakatifu cha Waislamu.
Katika mpango huo ambao umeanza kutekelezwa katika shule moja ya mji wa Siwan, nakala 50 za Qur’ani Tukufu iliyotarjumiwa kwa lugha ya Kihindi, zimesambazwa kwa Wahindu na watu wa dini nyinginezo.
Baada ya kugawanywa nakala hizo, gavana wa zamani wa jimbo la Bihar alihutubia hadhara hiyo akisema kuwa kitabu cha Qur’ani si kwa ajili ya Waislamu peke yao bali ni mwongozo kwa ajili ya wanadamu wote. Amesisitiza kuwa watu wote wana haki ya kusoma Qur’ani na kujifunza somo la maisha katika kitabu hicho.
Amesema Jamat Islamiya ya India inatayarisha tarjumi mpya ya Qur’ani kwa lugha ya Kihindi ambayo itatolewa kwa Wahindu ili kuwafahamisha ujumbe wa Uislamu. 801511