IQNA

Qur'ani kubwa zaidi iliyoandikwa kwa hati za mkono yaelekea kukamilika

18:37 - June 08, 2011
Habari ID: 2135133
Nakala kubwa zaidi ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa hati za mkono na msanii Muhammad Sabir Yaqut Hussaini wa Afghanistan itazinduliwa hivi karibuni.
Shirika la habari la Bakhtar News Agency limeripoti kuwa Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Afghanistan, na Mawaziri wa Wizara za Habari, Utamaduni, Hija na Wakfu wamekagua uandishi wa nakala hiyo ya Qur'ani na kuchunguza kwa karibu awamu zake ya mwisho.
Kazi ya kuandika nakala hiyo yenye thamani kubwa na ya aina yake ya Qur'ani inaendelea sasa kwa kipindi cha miaka mitano kwa ushirikiano wa taasisi ya Nasir Khosrou Balakhi yenye makao yeke mjini Kabul.
Hussaini Yaqut ni miongoni mwa wakimbizi wa Kiafghani waliokuwa nchini Iran na amekuwa akiandika Qur'ani hiyo katika makarasi ya mapambo. Msanii huyo anasaidiwa na taasisi ya Agha Khan nchini Afghanistan.
Msanii huyo anasema: "Kabla ya kuanza kuandika Qur'ani hii nilishauriana na maulamaa kadhaa wa Kiislamu kisha nikaanza kazi hii kwa kushirikiana na wasaidizi 10. 804596
captcha