Kwa mujibu wa gazeti la al-Ahram la Misri idara za wakfu na masuala ya Kiislamu katika mikoa tofauti ya nchi hiyo na Taasisi ya Abrar ambayo inashughulikia wagonjwa wa maradhi maalumu nchini humo tayari zimepokea majina ya watu wanaotaka kushiriki kwenye mashindano hayo.
Akizungumzia suala hilo, Muhammad Mahmoud Abu Hatab, mwakilishi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri mkoani Alexandria amesema kuwa lengo la kuandaliwa mashindano hayo ni kuwashajiisha walemavu wa akili waweze kuhifadhi Qur'ani, kunyanyua kiwango cha uelewa wa kidini miongoni mwao na kuwashirikisha katika nyanja mbalimbali za kijamii.
Watayarishaji wa mashindano hayo wanasema kuwa uandikishaji majina utaendelea kwa muda wa wiki moja na kwamba hakuna kizuizi chochote cha umri kwa wanaotaka kushiriki.
Washiriki watachuana katika makundi manne ya hifdhi ya sura fupi za A'la hadi an-Nas, hifdhi ya juzuu moja ya Qur'ani, hifdhi ya robo ya Qur'ani na hifdhi ya Qur'ani nzima. 806453