IQNA

Kikao cha kujadili uelewa mmbaya wa Qur'ani kufanyika Dubai

15:06 - June 12, 2011
Habari ID: 2136866
Taasisi ya Masuala ya Kheri na Kiislamu ya Dubai imepanga kufanya kikao maalumu siku ya Ijumaa tarehe 17 Juni kwa shabaha ya kujadili na kujibu maswali kuhusiana na mambo yasiyofahamika vyema na fikra potofu kuhusiana na baadhi ya mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa gazeti la Gulf Today kikao hicho kitafanyika katika makao ya Taasisi ya Masuala ya Kheri na Kiislamu ya Dubai IACA ambapo masuala 10 kati ya masuala yanayosababisha utata na kutoeleweka vyema katika Qur'ani Tukufu yatajadiliwa.
Kikao hicho ni sehemu ya warsha za masomo zinazoandaliwa na taasisi iliyotajwa kwa lengo la kunyanyua kiwango cha uelewa wa watu kuhusu masuala mbalimbali ya kidini na Kiislamu. Watayarishaji wa kikao hicho wanasema kuwa kitakuwa na athari kubwa katika kuondoa baadhi ya ufahamu na fikra potofu kuhusu Uislamu na mafundisho ya dini hii tukufu. Ufahamu mzuri wa Uislamu, kuondolewa tofauti zilizopo kati ya wafuasi wa dini tofauti, kusisitiza juu ya amani na kuishi pamoja kwa amani na wafuasi wa dini na jamii tofauti kwa msingi wa mafundisho mazuri ya Kiislami ni miongoni mwa malengo ya kufanyika kikao hicho. 806337
captcha