Kongamano hilo litafanyika sambamba na Mashindano ya 28 Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yatakayofanyika Juni 29 hadi Julai 4.
Kwa mujibu wa Shirika la Awqaf la Iran ambalo linaandaa mashindano hayo, wasomi wa kike wa Qur'ani, watafiti, walimu, waandishi na wengineo ni kati ya watakaoenziwa.
Kongamano hilo pia litawaenzi makari na mahafidh wa Qur'ani wa Iran walioshinda katika mashindano ya kitaifa na kimataifa. Kongamano la kuwaenzi wanaharakati wa kike wa Qur'ani pia lilifanyika mwaka jana pembizoni mwa mashindano ya 27 ya kimataifa ya Qur'ani.
807054