Akizungumzia suala hilo Abdallah bin Abdul Aziz al-Muslih Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo amesema kwamba vipindi hivyo vitarushwa hewani katika televisheni iliyotajwa ikiwa ni katika kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na wanazoni pamoja na washiriki wa kikao cha nane cha jumuiya hiyo kilichofanyika huko nchini Kuwait.
Kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa, jumuiya hiyo itakuwa ikizalisha thuluthi moja ya vipindi vyote vitakavyokuwa vikirushwa hewani na televisheni hiyo. Kwa mujibu wa mikataba iliyotiwa saini kati ya pande mbili, jumuiya hiyo itakuwa na nafasi muhimu katika utayarishaji wa vipindi vya televisheni hiyo ambavyo vitaanza kupeperushwa hewani mwanzoni mwa mwezi wa Shaaban.
Al-Muslih anasema kwamba huo ni mchango mdogo tu wa kuhudumia ujumbe wa kimaanawi wa Uislamu katika zama hizi. 808527