IQNA

Kipindi cha Taji la Qur'ani kutangazwa katika Kanali ya Qur'ani ya Algeria

18:08 - June 15, 2011
Habari ID: 2138969
Kanali ya Qur'ani ya Algeria itarusha hewani kipindi maalumu cha Tajul Qur'ani (Taji la Qur'ani) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kipindi hicho kitashughulikia masuala ya Qur'ani ya Kituo cha kidini cha Darul Imam cha mji wa Algiers.
Kazi ya kutayarisha kipindi hicho itaanza tarehe 20 Juni na wanafunzi zaidi ya 50 kutoka maeneo yote ya Algeria watashiriki katika shughuli hiyo na kuchuana katika kiraa ya Qur'ani.
Washindi 12 wa kwanza wa watachaguliwa na kupelekwa katika kituo maalumu ambapo watapata mafunzo ya dini na Qur'ani. 809343

captcha