Masomo ya hifdhi ya sura fupi za Qur'ani Tukufu na udhibiti wa sheria za tajwidi kwa mabinti wadogo walio na umri wa kati ya miaka 6 hadi 8 yamepangwa kuanza hapo kesho Jumatatu mjini Doha, Qatar na kuendelea kwa muda wa wiki tano.
Masomo hayo yanadhaminiwa na Taasisi ya Hifdhi na Mafunzo ya Qur'ani Tukufu ya al-Mimbar. Taasisi hiyo imetangaza kuwa mbali na masomo hayo ya tajwidi masomo mengine ya kidini na kiutamaduni yatatolewa kwa washiriki. Imeongeza kwamba mbali na kutolewa masomo hayo kwa mabinti walio na umri mdogo uliotajwa pia ina mipango ya kuandaa masomo kama hayo ya hifdhi ya Qur'ani kwa wanawake.
Taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2009 inaendesha shughuli zake chini ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar. 810955