IQNA

Majina ya washiriki katika warsha ya "Nuru na Kitabu" yaanza kusajiliwa Qatif

15:56 - June 19, 2011
Habari ID: 2140682
Shughuli ya kuandikisha majina ya washiriki katika warsha ya Nuru na Kitabu iliyopangwa kufanyika katika mji wenye wafuasi wengi wa madhehebu ya Shia wa Umm al Hammam katika mkoa wa Qatif nchini Saudi Arabia ilianza jana.
Warsha hiyo imetayarishwa na kamati ya wanawake wa Jumuiya ya masuala ya Qur'ani ya al Dhakiraat ya eneo la Umm Hammam mkoani Qatif.
Warsa hiyo itajadili aya mbili za 15 na 16 za suratul Maidah zinazosema: "Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anayekufichulieni mengi mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anayesamehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinachobainisha. Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoza kwenye njia iliyonyooka."
Warsa hiyo pia itakuwa na progamu ya nyimbo za qasida, makala za Qur'ani, uchoraji, kaligrafia ya Qur'ani na kadhalika. 810666

captcha