IQNA

Uteuzi wa jopo la majaji wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Iran

14:22 - June 22, 2011
Habari ID: 2142262
Jopo la majaji wa Mashindano ya 28 ya Qur’ani Tukufu ya Iran limeshateuliwa, amesema naibu mkuu wa Shirika la Wakfu la Iran.
Hujjatul Islam Ahmad Sharafkhani amesema kamati maalumu ilibunuwa kwa lengo la kuwateua majaji hao.
Baada ya mikutano kadhaa kamati hiyo ilitangaza kuwa wataalamu 16 wa Qur’ani kutoka Iran na nchi kadhaa wameteuliwa kama majaji. Nane kati yao ni kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Majaji hao ni pamoja na, kutoka Iran Abdol Rasul Abayi: mkuu wa jopo; Mohammad Reza Sotudenia: mkaguzi; Hojat-ol-Islam Haj Abol Ghasem: mtoaji muongozo kwa mahafidh; Hashem Roghani: kitengo cha Lahn; Ahmad Abol Ghasemi: kitengo cha ubora wa sauti; Hojat-ol-Islam Shahidipur: kitengo cha Waqf and Ibtida; Sayyid Mahdi Seyf: kitengo cha Tajweed; na Amir Aghayi: kitengo cha hifdhi sahihi.
Wengine katika jopo la majaji ni: Fakhruddin Sarumpaet kutoka Indonesia, Azhar Ibn Uthman kutoka Malaysia, Yahya Muhamamd Ali Hassan kutoka Iraq, Saeedi Yusuf kutoka Algeria, Hussein Hamdan kutoka Syria, Ahmed Isa Hussein Al-Ma’sarawi kutoka Uturuki na Muhammad Amin Mashali kutoka Syria.
Karii maarufu wa Misri Abdulfattah Taruti atakuwa mgeni wa heshima na vilevile ataongoza kozi kadhaa kuhusu kiraa. Mashindano ya mwaka huu ya Qur’ani Tukufu ya Tehran yatakayoanza tarehe 27 Rajab yatajumuisha makarii na mahafidh 99 kutoka nchi 53.
812565
captcha