Kwa mujibu wa gmanews, Qur'ani hizo ambazo zimeandikwa kwa maandishi makubwa zimelenga kuwasaida watu walio na umri mkubwa waweze kusoma kwa urahisi kitabu hicho kitakatifu.
Mbali na Qur'ani hizo Waislamu hao pia wametuma nchini kwao kilo 2000 za tende na miswala ili kutumiwa na wenzao wakati wa ibada muhimu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Msaada huo wa Wafilipino ambao unatolewa kwa mara ya pili katika kipindi cha mwaka huu, unatekelezwa kutokana na ushauri wa mshauri mkuu wa Wafilipino katika Idara ya Masuala ya Kiislamu ya Dubai. 812083