Maonyesho hayo ambayo ni ya pili kuwahi kufanyika nchini humo na ambayo yameandaliwa na Wizara ya Utamaduni ya nchi hiyo yamepangwa kufanyika tarehe 25 hadi 28 za mwezi huu wa Juni. Akizungumzia jambo hilo Majid Hamid al-Yatim, mwakilishi wa wizara iliyotajwa amesema kuwa baadhi ya athari zitakazoonyeshwa katika maonyesho hayo ni pamoja na mabango adimu 135 yanayohusiana na uandishi wa mkono pamoja na chapa nchini Yemen, na mengine 16 yanayohusiana na mwenendo wa ukarabati wa nuskha za Qur'ani zilizoandikwa kwa mkono nchini humo.
Mwakilishi huyo ameiomba sekta binafsi kuwekeza katika uvumbuzi wa athari za maandishi ya mikono, uhifadhi wa athari hizo na vilevile kuzuia uuzaji wa magendo wa nuskha za kale zilizoandikwa kwa mkono za nchi hiyo nje ya nchi. Ametaja masuala hayo kuwa moja ya malengo muhimu ya kufanyika maonyesho hayo. 812857