IQNA

Vikao vya al Fatiha kwa ajili ya Ustadh Shoaisha Kufanyika Iraq

16:20 - June 26, 2011
Habari ID: 2144713
Darul Qur'an al-Kareem ya mjini Nassiriyya katika jimbo la Dhiqar imeandaa vikao vya Fatiha hii leo Jumapili kwa ajili ya kukumbuka na kumuombea dua Abulainain Shoaisha Sheikh wa Makarii wa Misri aliyeaga dunia hivi karibuni.
Akibainisha suala hilo, Ra'd Adnan an-Nasiri mkuu wa kituo hicho cha Qur'ani amesema kuwa vikao hivyo vitafanyika kwa kuhudhuriwa na viongozi na maafisa wa kieneo wa mkoa huo. Amesema wasomaji Qur'ani wa mkoa huo waliovutiwa na kuiga kisomo cha Qur'ani cha Sheikh Shoaisha wamealikwa pia kushiriki kwenye vikao hivyo ili kuwakumbusha washiriki sauti na kisomo cha kuvutia cha marehemu huyo.
Sheikh Shoaisha ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Makarii wa Misri aliaga dunia siku ya Alkhamisi iliyopita tarehe 24 Juni.
captcha