IQNA

Nchi 50 zatangaza kuwa tayari kushiriki mashindnao ya kimataifa ya Qur'ani Dubai

18:30 - July 03, 2011
Habari ID: 2148284
Wawakilishi wa nchi 50 na Waislamu wanaoishi katika nchi zisizokuwa za Kiislamu duniani wametangaza kuwa wako tayari kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani zawadi ya Dubai.
Mwenyekiti wa Kitengo cha Masuala ya Uendeshaji na Fedha cha Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai Abdurahim Hussain amesema kuwa hadi kufikia Alkhamisi iliyopita wawakilishi wa nchi 50 na Waislamu wanaoishi katika nchi mbalimbali duniani walikuwa tayari wametangaza kwamba wako tayari kushirki mashindano ya mwaka huu ya Qur'ani ya Dubai yatakayofanyika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Abdurahim Hussain amesema fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo bado ipo na kuongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika katika viwango vya hifdhi ya Qur'ani nzima.
Ameongeza kuwa mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya dirhamu laki mbili na nusu, mshindi wa pili dirhamu laki mbili, mshindi wa tatu dirhamu laki moja na nusu, mshindi wa nne dirhamu elfu 65 za Imarati. Anesena kuwa washiriki wote wa mashindano hayo ambao hawatafanikiwa kushinda watapewa zawadi ya dirhamu elfu 30. 818959
captcha