IQNA

Warsha ya mafunzo ya "Kuelekea kwenye Qur'ani" kufanyika Afrika Kusini

20:36 - July 03, 2011
Habari ID: 2148289
Warsha ya mafunzo ya "Kuelekea kwenye Qur'ani Tukufu: Kiraa Hadi kwenye Taqwa" itafanyika Cape Town nchini Afrika Kusini katika kipindi cha kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
kituo cha habari cha CTME kimeripoti kuwa warsha hiyo ya mafunzo itafanyika katika msikiti wa Dar al Naeem mjini Cape Town tarehe 10 Julai na itaendelea ka kipindi cha wiki nne. Wanawake wa Kiislamu watapewa mafunzo kuhusu maudhui mbalimbali zinazohusiana na Qur'ani katika warsha hiyo.
Tarehe 3 Julai pia Baraza la Sheria la Waislamu la Jumuiya ya Masuala ya Qur'ani ya Afrika Kusini litakuwa na kikao cha kukhitimisha Qur'ani kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Baadhi ya mahafidhi, walimu wa Qur'ani na wapenzi wa kitabu hicho watasoma juzuu za kuanzia 26 hadi 30 za kitabu hicho kitakatifu. 818661
captcha