IQNA

Karii wa Sudan:

Kuhifadhi Qur'ani kunawalinda vijana mbele ya upotofu wa kifikra

10:28 - July 04, 2011
Habari ID: 2148550
Ninatarajia kuona siku ambayo vijana wote wa Kiislamu watahifadhi Qur'ani Tukufu, kwani kuhifadhi kitabu hicho ha Mwenyezi Mungu na kuelewa maana ya aya zake kunawarekebisha vijana na kuwalinda mbele ya opotofu wa kifikra, kimaadili na kijamii.
Hayo yamesemwa na al Ghali Ismail Issa, karii na mwakilishi wa Sudan katika kitengo cha kiraa cha Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran. Amesema kuwa jamii yenye vijana waliohifadhi Qur'ani na kuelewa maana ya aya zake huwa jamii ya Kiislamu, safi na iliyopata mafunzo bora ambayo inaweza kutambua njia nyoofu kwa kutegemea kitabu hicho kitukufu.
al Ghali Issa amesema: "Ninawausia vijana Waislamu hususan vijana wa Iran kuipa Qur'ani Tukufu umuhimu mkubwa zaidi kwani jamii yenye vijana walioshikamana na Qur'ani haiwezi kuondoka katika njia sahihi na inapokaribia kupotea njia hupata mwongozo wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu na kurejea".
Karii huyo wa Sudan amesema hii ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran. Kuhusu kiwango cha mashindano haya amesema kwamba, yanafanyika katika viwango vya juu na amelishukuru Shirika la Wakfu la Iran kwa kazi nzuri ya kuandaa mashindano hayo.
Issa amesema siku ya kwanza ya Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran iliwavutia na kuwashangaza wengi kutokana na kiraa nzuri kupita kiasi.
Amesema kuwa ushindani katika mashindano ya sasa ya Qur'ani mjini Tehran ni mkubwa mno lakini amesisitiza kuwa ana matumaini ya kushinda nafasi za kwanza. 819269
captcha