Katika siku za hivi karibuni nchini Misri kumesambazwa nakala za Qur'ani Tukufu ambazo zimepambwa kwa rangi mbali mbali katika maduka nchini humo hasa pembizoni mwa Chuo Kikuu cha Al Azhar. Wamisri wammeshangazwa na nakala hizo za Qur'ani huku taasisi na viongozi wa Kiislamu wakilaani uchapishaji wa nakala hizo ambazo hazina maelezo kuhusu mchapishaji. Al Azhar imeitisha kikao cha dharura kufuatilia kadhia hiyo.
{$sepehr_old_album_3444842}