IQNA – Uwanja wa Sala (Musalla) wa Imam Khomeini (RA) mjini Tehran umekuwa uwanja wa kukutania nyoyo zilizokusanyika kati ya tarehe 4 na 5 Julai, 2026, kwa ajili ya kumuaga kwa heshima za mwisho Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake, walimiminika kutoka kila pembe ya nchi kutoa buriani kwa machozi na nyoyo zilizojawa na uzito wa hisia kwa baba ambaye amekuwa nguzo na kimbilio la taifa hili kwa miaka mingi. Katika saa hizi za majonzi, Musalla haukuwa tu mahali pa kawaida; ulikuwa simulizi hai ya machozi, uaminifu usiotikisika, na ahadi mpya ya taifa lililomsindikiza Kiongozi wake Shahidi kuelekea katika pumziko lake la milele.