IQNA

Sikiliza adhana iliyorekodiwa mwaka 1885 katika Msikiti Mtakatifu wa Makka

21:35 - November 25, 2020
Habari ID: 3473392
TEHRAN (IQNA)- Adhana ya kale zaidi kuwahi kurekodiwa katika Msikiti Mtakatifu wa Makka (Al Masjid al-Haram) inaaminika kurekodiwa miaka 140 iliyopita.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, adhana hii ilirekodiwa mwaka 1885 na msomi wa masuala ya mashariki (Mustashriqeen) kutoka Uholanzi Christiaan Snouck Hurgronje.

Mkanda asili wa adhana hiyo umewekwa katika Chuo Kikuu cha Leiden mjini Leiden nchini Uholanzi. Hatahivyo jina la muadhini huyo halijulikani.

Snouck Hurgronje (1857 – 1936), alikuwa msomi wa tamaduni na lugha za mashariki na mshauri wa utawala wa kikoloni wa Uholanzi nchini Indonesia. Msomi huyo wa Uholanzi alikuwa akizungumza lugha ya Kiarabu kikamilifu na kupitia gavana wa utawala wa Othmaniya mjini Jeddah, aliruhusiwa kuelekea Makka mwaka 1884 baada ya kusilimu na kupewa jina la Abd al-Ghaffar al-Laydini.

na inadokezwa kuwa alikuwa miongoni mwa wasomi wa kwanza wan chi za Magharibi kufika Makka na kuusoma Uislamu kitaalamu.

Sikiliza hiyo adhana hapa chini.

3937068

 

captcha