IQNA

Lita milioni 1.5 za maji ya Zamzam zimetuma Makka miezi mitatu

22:06 - November 22, 2020
Habari ID: 3473383
TEHRAN (IQNA) – Waislamu walioutembelea Msikiti Mtakatifu wa Makka (Masjid al-Haram) katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita wametumia lita milioni 1.5 za maji ya Zamzam.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na gazeti la Okaz, halikadhaloika lita milioni 1.8 za maji ya Zamzam zimetumika tokea mwanzo wa mwaka huu wa 1432 Hijria Qamaria, ambao ulianza Agosti 20.

Saudia iliurhusu tena ibada ya Umrah kuanzia Oktoba 4 baada ya Msikiti Matakatifu wa Makka kufungwa kwa tarkibani miezi saba kutokana na janga la corona. Hivi sasa Waislamu kutoka nje ya Saudia wanaruhusiwa kufika katika mji wa Makka kwa ajili ya ibada ya Umrah.

Kila siku wakuu wa Saudia hutekeleza oparesheni za kusafisha eneo hilo takatifu kwa kutumia dawa za kuangamiza virusi.

Waislamu wanaamini kwamba maji yanayotoka katika visima vya zamzam vinavyopatikana katika Msikiti Mtakatifu wa Makka yana utukufu na baraka telele na hivyo kila anayetembelea msikiti huo mtakatifu hujitahidi kuyapata maji hayo kwa ajili ya kunywa na kuwapelekea wengine kama zawadi.

3473189

Kishikizo: zamzam umrah makka
captcha